42. Majina mabaya yanatakiwa kubadilishwa

Uokozi kutokamana na majina ya haramu na yaliyochukizwa ni kuyabadili kwa majina yaliyowekwa katika Shari´ah na yenye kujuzu. Mabadilisho yanatakiwa kupitika kupitia amri ya mlezi anayetambulika Kishari´ah. Yeye ndiye anatakiwa kumuamrisha yule mpewa jina mpungufu au ambaye kishabaleghe na kupevuka kubadili jina.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alibadilisha majina ya watu wengi; alibadili majina ya kishirikina na majina ya kikafiri kwenda majina ya kiumini. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akibadilisha majina mabaya kwa majina mazuri.”

Ameipokea at-Tirmidhiy.

Atalijua hilo mwenye kusoma kitabu “al-Iswaabah fiy Tamyiyz Asmaa´is-Swahaabah” cha Ibn Hajar.

Udhahiri ni kwamba mwongozo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa kubadili jina kwa matamko ya kufanana. Kwa mfano alibadili Shihaab kwenda Hishaam na Juthaamah kwenda Hassaanah.

Hali kadhalika ´Abdun-Nabiy linatakiwa kubadilishwa kwenda ´Abdul-Ghaniy, ´Abdur-Rasuul kwenda ´Abdul-Ghaniy, ´Abdu ´Aliy kwenda ´Abdul-´Aliy, ´Abdul-Husayn kwenda ´Abdul-Muhsin, Hanash kwenda Anas, ´Abdul-Kaadhwim kwenda ´Abdul-Qaadir na kadhalika. Lililo muhimu ni kubadilisha jina kwenda katika jina lililopendekezwa au linalojuzu[1].

[1] Miftaah Daar-is-Sa´aadah, uk. 259.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 18/03/2017