42. Dalili ya ishirini kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

43- ´Abdullaah bin al-Haarith ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah ameumba vitu vitatu kwa mkono Wake: Amemuumba Aadam kwa mkono Wake, ameiandika Tawraat kwa mkono Wake na ameipanda Pepo kwa mkono Wake.”[1]

Kuna Swahabah anayekosa katika cheni ya wapokezi.

Hadiyth inafahamisha kuwa uandishi umeumbwa, bi maana uandishi wa Tawraat umeumbwa. Kuhusu kile chenye kuandikwa ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall).”

[1] al-Bayhaqiy (692) na Abush-Shaykh (5/1555).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 09/07/2019