42. Dalili ya arubaini kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

40- Muhammad ametukhabarisha: Ahmad ametuhadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: Na Sulaymaan bin Ahmad ametuhadithia: al-Muqdaam bin Daawuud ametuhadithia: Asad bin Muusa ametuhadithia: Yuusuf bin Ziyaad ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Mun´im bin Idriys, kutoka kwa babu yake Wahb bin Munabbih, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:

“Kuna myahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Je, Allaah amejificha na viumbe Wake kwa kitu kingine kisichokuwa mbingu?” Akasema: “Ndio. Kati Yake na Malaika ambao wameizunguka ´Arshi kuna pazia sabini za nuru,  pazia sabini za moto, pazia sabini za viza, pazia sabini za mito ya hariri, pazia sabini za hariri nyororo, pazia sabini za lulu nyeupe, pazia sabini za  nyekundu, pazia sabini za manjano, pazia sabini za kijani, pazia sabini za mwanga unaotoka kwenye mwanga wa moto na nuru, pazia sabini za theluji, pazia sabini za maji, pazia sabini za mawingu, pazia sabini za mvua kali na pazia sabini za ukubwa wa Allaah usielezeka.” Akasema: “Nieleze kuhusu Malaika aliye karibu Naye?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Umenisadikisha kwa yale niliyosema, ee myahudi?” Akasema: “Ndio.” Ndipo akasema: “Malaika aliye karibu Naye ni Israafiyl, kisha Jibriyl, kisha Mikaaiyl halafu Malaika wa mauti.”[1]

[1] Ibn-ul-Jawziy amesema:

”Hadiyth amezuliwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Abdul-Mun´im ametuhumiwa. Ahmad na Yahyaa wamemtuhumu uongo. ad-Daaraqutwniy amesema: ”Yeye na baba yake wote wawili ni wenye kuachwa.” (al-Mawdhuu´aat (1/117))

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 136-137
  • Imechapishwa: 20/06/2018