42. Dalili juu ya vidole vya Allaah

42- Abu Muhammad Yahyaa bin Muhammad bin Swaa´id ametusomea: Fudhwayl bin ´Iyaadhw ametuhadithia, kutoka kwa Sulaymaan (bin al-A´mash), kutoka kwa Abu Sufyaan, kutoka kwa Anas bin Maalik aliyesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema: “Ee Mwenye kuzigeuza nyoyo. Uthibitishe moyo wangu katika dini Yako.” Wakasema: “Unachelea juu yetu ilihali tumekuamini na tumekuwa na yakini juu ya yale uliyokuja nayo kwetu?” Akasema: “Ni kipi kinachonijuza? Hakika nyoyo za viumbe ziko kati ya vidole viwili katika vidole vya Allaah (´Azza wa Jall).”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 88-90
  • Imechapishwa: 31/03/2018