al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akifasiri Aayah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً

“Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu kikamilifu.” (02:208)

“Bi maana uongozi wa Kiongozi wa waumini.”[1]

Baatwiniy huyu tunamwambia ya kwamba Aayah hii Allaah Anawaamrisha waumini watendee kazi mambo yote yaliyowekwa katika Shari´ah katika imani na Uislamu. Lakini hata hivyo Baatwiniy huyu amesafisha maana ya Aayah kwa tafsiri yake. Iko wapi imani kumuamini Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Kuko wapi kusimamisha Shari´ah za Kiislamu?

[1] Tafsiyr al-Qummiy.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 77
  • Imechapishwa: 19/03/2017