41. Mume amkinge mke wake na Moto

Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake yeye awe ni sababu ya kumuokoa na Moto kwa kumfundisha, kumuamrisha mema, kumkataza maovu na kuwa na subira juu ya hilo. Amzuie na yale ambayo yanaweza kuwa ni sababu ya yeye kuingia Motoni. Allaah (´Azza wa Jall) Amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ

“Enyi mlioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na Moto [ambao] mafuta [kuni] yake ni watu na mawe.”[1]

Mola Wetu (Subhaanahu wa Ta´ala) Amesema pia:

وَأْمُرْ أَهْلَكَ بِالصَّلَاةِ وَاصْطَبِرْ عَلَيْهَا

“Na amrisha ahli zako Swalah na dumisha kusubiri kwayo.”[2]

[1] 66:06

[2] 20:132

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 58
  • Imechapishwa: 24/03/2017