41. Maswahabah bora baada ya wale watatu

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Baada ya hawa watatu ni wale wa mashauriano watano: ´Aliy bin Abiy Twaalib, az-Zubayr, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, Sa´d na Twalhah. Wote walikuwa wanastahiki ukhaliyfah na wote walikuwa viongozi. Dalili yetu juu ya hilo ni maneno ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Tulikuwa, ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yuhai,  tukizingatia ya kwamba Abu Bakr ndiye bora na halafu ´Umar, kisha ´Uthmaan. Kisha tunanyamaza.”

Hapa ametajwa Sa´d, katika baadhi ya nusukha ametajwa Sa´iyd. Kwa hali zote mbili wanatimiza idadi ya sita. Imaam Ahmad amesema:

“Wote walikuwa wanastahiki ukhaliyfah… “

Tazama makadirio ya Imaam Ahmad. Kwa nini aseme hivo? Kwa kuwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) aliwateua watu hawa na kusema kwamba yule atakayeteuliwa kuwa khaliyfah ndiye atakuwa khaliyfah. Kutokana na uteuzi wa ´Umar ndio Ahmad akasema kuwa wote ni viongozi na kwamba wote wanastahiki ukhaliyfah. Imaam Ahmad amesema:

Dalili yetu juu ya hilo ni maneno ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Tulikuwa, ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yuhai,  tukizingatia ya kwamba Abu Bakr ndiye bora na halafu ´Umar, kisha ´Uthmaan. Kisha tunanyamaza.”

Baada ya watu wa mashauriano wanakuja Muhaajiruun walioshiriki katika vita vya Badr, kisha Answaar walioshiriki katika vita vya Badr; kila mmoja kwa mujibu wa kuhajiri na kutangulia kwake katika Uislamu.”

Kama mnavyojua kupitia tafiti za kisomi za Ahl-us-Sunnah mnajua ya kwamba ´Aliy bin Abiy Twaalib ana fadhila nyingi, alipewa kiapo cha usikivu na utiifu na Maswahabah walimchagua na kumpa kiapo cha usikivu. Anakuja nafasi ya nne kutokamana na mpangilio wa ukhaliyfah na fadhila. Imaam Ahmad amesema:

“Baada ya watu wa mashauriano wanakuja Muhaajiruun walioshiriki katika vita vya Badr, kisha Answaar walioshiriki katika vita vya Badr; kila mmoja kwa mujibu wa kuhajiri na kutangulia kwake katika Uislamu.”

Wako wanachuoni wenye kuonelea kuwa wale waliokula kiapo ´Aqabah ni bora kuliko wale walioshiriki katika vita vya Badr. Wengi ambao walikula kiapo ´Aqabah walishiriki katika vita vya Badr.

Wale walioshiriki vita vya Badr wanatofautiana kati yao na wale waliokula kiapo ´Aqabah wanatofautiana kati yao. Muhaajiruun wanatofautiana kati yao na Answaar wanatofautiana kati yao kwa mujibu wa fadhila, elimu na kujitolea kwao katika Uislamu mali na nafsi zao.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 412
  • Imechapishwa: 10/10/2017