41. Kursiy imezizunguka mbingu na ardhi

Kursiy imeumbwa na iko chini ya ´Arshi. ´Arshi ni kubwa zaidi kuliko yenyewe. Kursiy imezizunguka mbingu na ardhi. Ikiwa huu ndio ukubwa wa Kursiy, tuseme juu ya ´Arshiy? Tusemeje juu ya ukubwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)! Fikira na mawazo hayawezi kulifikiria hilo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hazikuwa mbingu saba ukilinganisha na Kursiy isipokuwa ni kama dirhamu saba zilizowekwa kwenye ngao ya vita. Kursiy ukiilinganisha na ´Arshi si kitu isipokuwa ni kama mfano wa kijipete cha chuma kilichotupwa katika uwanja mkubwa.”[1]

Haya yanajulisha juu ya ukubwa wa Allaah – vipi kuhusu ukubwa wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)!

Kursiy iko juu ya mbingu. Juu ya mbingu zipo bahari, juu ya bahari ipo Kursiy, juu ya Kursiy ipo ´Arshiy na juu ya ´Arshi yuko Allaah ambaye amelingana juu yake. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu ya viumbe Wake. Licha ya ujuu na kungatika Kwake hakuna chochote ardhini wala mbinguni kinachofichikana Kwake. Anakijua kila kitu na hakuna chochote kinachofichikana Kwake:

وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّةٍ فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ

“Kwake zipo funguo za mambo yaliyofichikana; hakuna azijuaye isipokuwa Yeye tu na anajua yale yote yaliyomo barani na baharini na halianguki jani lolote isipokuwa hulijua na wala punje katika viza vya ardhi na wala kilichorutubika na wala kikavu isipokuwa kimo ndani ya Kitabu kinachobainisha wazi.”[2]

[1] Ibn Abiy Shaybah katika ”Kitaab-ul-´Arsh” (58), Ibn Hibbaan (361), Abuush-Shaykh (259) na wengineo. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (109).

[2] 6:59

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 27/07/2021