41. Jahmiyyah, Mu´tazilah na vifaranga vyao wameangamia


Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

14- Wameyapokea hayo watu zisizorudishwa Hadiyth zao

     wameangamia watu waliowakadhibisha na wakebehewe

MAELEZO

Wameyapokea hayo watu… – Wamepokea Hadiyth kuhusu Kushuka kundi la Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

… zisizorudishwa Hadiyth zao – Kwa sababu ni Hadiyth zilizopokewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Jahmiyyah na wakanushaji hawana njia yoyote inapokuja katika mlolongo wa wapokezi.

wameangamia watu… – Kwa kuwa wamekadhibisha Hadiyth hizi na wakapinga kuwa Allaah anashuka na wakapindisha maana ya Hadiyth za Mtume kinyume na alivyokusudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wamemzulia na kumsemea Allaah uongo.

… waliowakadhibisha na wakebehewe – Nao ni Jahmiyyah na wale wenye kufuata mfumo wao. Asli ya balaa ni Jahmiyyah na Mu´tazilah. Wote waliokuja baada yao wakafuata mfumo wao. Wao ndio ambao wamefungua mlango wa upotevu. Wapotevu wote waliokuja baada yao ni wenye kuwafuata. Wanaguswa na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kuita katika upotevu atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya ambaye atamfuata, hakutopungua kitu katika madhambi yao, na mwenye kulingania katika uongofu atakuwa na ujira mfano wa ujira wa ambaye atamfuata, hakutopungua kitu katika ujira wao.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7321) na Muslim (16) na (2674)