29. ´Ibaadah ya mwanamke ambaye mimba imeporomoka ndani ya miezi mitatu

Swali 29: Mimi ni mwanamke ambaye mimba yangu imeporomoka ndani ya mwezi wa tatu mwaka mmoja uliopita na sikuswali mpaka niliposafika. Nimeambiwa kwamba nilipaswa kuswali. Nifanye nini na mimi sijui idadi halisi ya siku?

Jibu: Kinachofahamika kwa wanachuoni ni kwamba mwanamke akiporomosha mimba ya miezi mitatu haswali. Kwa sababu mwanamke akiporomosha kipomoko ambaye tayari amekwishabainisha umbile la mtu basi damu inayomtoka inazingatiwa kuwa ni damu ya uzazi. Hivyo hatoswali. Wanachuoni wamesema kwamba umbile la mtu kutoka kwenye kipomoko hicho linaweza kubainika pale kinapotimiza siku 81. Kipindi hichi ni chini ya miezi mitatu. Kama una uhakika kwamba mimba iliporomoka ndani ya miezi mitatu, basi damu aliyopata ni damu ya kawaida ambayo hatakiwi kuacha swalah kwa ajili yake.

Ni lazima kwa dada huyu muulizaji ajikumbushe mwenyewe. Ikiwa kipomoko kimetoka kabla ya siku 81, basi anatakiwa kulipa swalah zake. Akiwa hajui ni swalah ngapi ameacha basi atatakiwa kujitahidi na alipe kwa mujibu wa vile inavyomtilia nguvu dhana yake kwamba hakuswali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 26
  • Imechapishwa: 27/07/2021