9- Mwanamke akiwa ni mwenye kunyonyesha au mwenye mimba na akachelea juu ya nafsi yake au juu ya mtoto kutokana na kufunga, basi atakula. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Anas bin Maalik al-Ka´biy (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemwondoshea msafiri nusu ya swalah na swawm kwa msafiri, mjamzito na mnyonyeshaji.”

Wameipokea watano. Hili ni tamko la Ibn Maajah[1].

Ni lazima kwake kulipa kwa idadi ya siku alizokula pale atapokuwa na wepesi wa kufanya hivo na akaondokwa na khofu kama mgonjwa atapopona.

[1] Ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 58
  • Imechapishwa: 09/05/2020