41. Dalili ya thelathini na tisa kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

39- Muhammad ametukhabarisha: Hamad ametuhadithia: Ahmad ametuhadithia: Abu ´Amr bin Hamdaan ametuhadithia: al-Hasan bin Sufyaan ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Umar bin Abaan ametuhadithia: Marwaan bin Mu´aawiyah ametuhadithia, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Abdillaah, kutoka kwa Yaziyd bin al-Aswamm, kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Malaika aliyepewa kazi ya kupuliza parapanda hajapatapo kuacha kuangalia kuielekea ´Arshi kwa kuchelea asije kuamrishwa kabla ya kuwahi kurudisha kupepesa macho kwayo. Macho yake yanaangaza kama nyota mbili zinazomeremeta.”[1]

[1] al-Haakim (4/559) aliyesema:

”Mlolongo wa wapokezi wa Hadiyth ni Swahiyh.”

Ameafikiwa na adh-Dhahabiy aliyeongeza:

”Iko juu ya masharti ya Muslim.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 133-134
  • Imechapishwa: 18/06/2018