41. Baadhi ya hukumu zinazomuhumu mwanamke katika Hajj na ´Umrah II

4 – Mwanamke atapopata hedhi au damu ya uzazi kwenye njia yake ya kwenda hajj, basi ataendelea na safari yake. Ikimpata wakati atapokuwa kwenye Ihraam, basi atafanya Ihraam kama wanawake wengine waliowasafi. Kwa sababu ile nafsi ya Ihraam haishurutishi twahara. Mtunzi wa “al-Mughniy” amesema:

“Jumla ya hayo ni kwamba kuoga ni jambo limesuniwa kwa wanawake wanapokuwa Ihraam kama ilivyosuniwa kwa wanaume. Kwa sababu ni ´ibaadah na imekokotezwa zaidi kwa mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kwa kupokelewa Hadiyth juu yao. Jaabir amesema: “Mpaka tulipofika Dhul-Hulayfah ambapo Asmaa´ bint ´Umays akamzaa Muhammad bin Abiy Bakr akamtumaa [mtu] kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimuuliza ni kipi afanye. Akasema: “Oga, jifunike kwa nguo na hirimia.”[1]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwmaba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke mwenye damu ya uzazi na mwenye hedhi wakifika katika wakati wake watahirimia na watatekeleza ´ibaadah zote isipokuwa kutufu kwenye Ka´bah.”

Ameipokea Abu Daawuud.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha ´Aaishah kuhirimia ilihali yuko na hedhi.”

Hekima kwa mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kuoga ni kwa ajili ya kujisafisha na kukata ile harufu mbaya kwa ajili ya kuondosha maudhi kwa watu wakati wanapokusanyika na kupunguza najisi. Wakipatwa na hedhi au nifasi wakati wako wanafanya Ihraam, haitoathiri Ihraam yao. Ikiwapata hedhi ilihali ni wenye kuhirimia hajj ya ´umrah hayo hayatoathiri Ihraam yao na watajiepusha na mambo yaliyoharamishwa katika Ihraam. Wasitufu kwenye Ka´bah mpaka kwanza watwahirike kutokamana na hedhi na nifasi na waoge.

Ikifika siku ya ´Arafah na hawajatwahirika na wakawa wamehirimia ´umrah hali ya kufanya Tamattu´ kwa ´umrah kwenda hajj, basi watahirimia hajj na wataingiza hajj ndani ya ´umrah na watakuwa ni wenye kufanya Qiraan. Dalili juu ya hayo ni kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alipata hedhi na alikuwa amehirimia ´umrah akaingia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na huku analia akasema: “Ni kipi kinachokuliza; pengine umepata hedhi?” Akasema: “Ndio.” Akasema: “Hiki ni kitu ambacho Allaah amewaandikia wana wa Aadam. Fanya yale anayofanya mwenye kuhiji isipokuwa tu usifanye Twawaaf kwenye Nyumba mpaka utwahirike.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Katika Hadiyth ya Jaabir iliopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim:

“Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaingia ndani kwa ´Aaishah na akamkuta analia. Akasema: “Ni lipi jmbo lako?” Akasema: “Jambo langu ni kwamba nimepata hedhi na watu wamekwishahirimia na mimi sijahirimia na sijafanya Twawaaf kwenye Ka´bah. Hivi sasa watu wanaenda katika hajj.” Akasema: “Hiki ni kitu ambacho Allaah amewaandikia wana wa Aadam. Oga, kisha hirimia.” Akafanya hivo na akasimama sehemu zote mpaka alipotwahirika akatufu Ka´bah na [akatembea] Swafaa na Marwah kisha akasema: “Umeshatokana na hajj yako na ´umrah yako vyote viwili… “

´Allaamah Ibn-ul-Qayyim amesema “Tahdhiyb-us-Sunan”:

“Hadiyth ni Swahiyh na zinasema wazi kwamba amehirimia kwa ´umrah kwanza kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha ahirimie hajj; akawa ni mwenye Qiraan. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Inakutosha kufanya Twawaaf kwenye Ka´bah na baina ya Swafaa na Marwah kwa ajili ya hajj na ´umrah yako.”[2]

[1] (03/93-294).

[2] (03/293-294).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 12/11/2019