41. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa kumi na mbili wa al-Baqarah

al-´Ayyaashiy amesema wakati alipokuwa anafasiri Aayah:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ مِن بَعْدِ مَا بَيَّنَّاهُ لِلنَّاسِ فِي الْكِتَابِ ۙ أُولَـٰئِكَ يَلْعَنُهُمُ اللَّـهُ وَيَلْعَنُهُمُ اللَّاعِنُونَ

“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na uongofu baada ya kuwa Tumeyabainisha kwa watu katika Kitabu, hao Anawalaani Allaah na wanalaaniwa na kila mwenye kulaani.” (02:159)

“Ibn Abiy ´Umayr amepokea kutoka kwa yule aliyemtaja kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ

“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na uongofu… “

“Inahusiana na ´Aliy.”

Abu Ja´far amesema kuhusu:

إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلْنَا مِنَ الْبَيِّنَاتِ وَالْهُدَىٰ

“Hakika wale wanaoficha yale Tuliyoyateremsha katika hoja bayana na uongofu… “

“Anakusudia sisi.”

Halafu akapokea kwa mnyororo mwingine ya kwamba Abu ´Abdillaah amesema:

“Sisi ndio wenye kukusudiwa.”[1]

Hakika Aayah inahusiana wazi wazi na yule mwenye kuficha chochote katika yale Aliyoteremsha Allaah. Haijalishi kitu sawa ikiwa kinahusiana na Tawhiyd, ´ibaadah, ya halali, ya haramu au mambo mengine yaliyowekwa katika Shari´ah kwenye Qur-aan, Tawrat au Injiyl. Mfano wa hayo ni mayahudi na manaswara walificha unabii wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sifa zake katika vitabu viwili. Kisha Baatwiniy huyu anajaribu kubadili maana kubwa ya Aayah hii kwenda katika maslahi ya ´Aqiydah yake ambayo haisapotiwi na Qur-aan wala na Sunnah kwa njia yoyote ile.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/71-73).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 75-76
  • Imechapishwa: 19/03/2017