71- Swafwaan bin ´Assaal al-Muraadiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo alikuwa msikitini hali ya kuwa ameshegama kwenye blanketi yake nyekundu. Nikamwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Mimi nimekuja kutafuta elumu.” Akasema: “Karibu ee mwanafunzi. Hakika mwanafunzi anazungukwa na Malaika na wanamfunika kwa mbawa zao. Kisha wanapandiana mpaka wanafika kwenye mbingu ya chini kwa ajili ya kupenda kwao kile anachokitafuta.”[1]

Ameipokea Ahmad, at-Twabaraaniy kwa cheni ya wapokezi nzuri na tamko ni lake, Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake na al-Haakim amesema:

“Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh.”

Ibn Maajah amepokea mfano wake kwa ufupi.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/139-140)
  • Imechapishwa: 14/09/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy