40. Fadhila za Maswahabah


Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“Mbora wa Ummah huu baada ya Mtume wake ni Abu Bakr as-Swiddiyq, kisha ´Umar bin al-Khattwaab halafu ´Uthmaan bin ´Affaan. Tunawatanguliza hawa watatu kama walivyotangulizwa na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hawakutofautiana juu ya hilo.”

MAELEZO

Mlango huu unahusiana na fadhila za Maswahabah. Fadhila za Maswahabah zimethibiti katika Qur-aan, Sunnah na maafikiano ya waislamu. Wapotevu tu katika Khawaarij na Raafidhwah ndio wanaonelea kinyume. Qur-aan inawasifu na inabainisha hadhi na nafasi zao. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ

“Wale waliotangulia mwanzoni miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao, nao wameridhika Naye na Amewaandalia mabustani yapitayo chini yake mito – ni wenye kudumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.”[1]

لَا يَسْتَوِي مِنكُم مَّنْ أَنفَقَ مِن قَبْلِ الْفَتْحِ وَقَاتَلَ ۚ أُولَـٰئِكَ أَعْظَمُ دَرَجَةً مِّنَ الَّذِينَ أَنفَقُوا مِن بَعْدُ وَقَاتَلُوا ۚ وَكُلًّا وَعَدَ اللَّـهُ الْحُسْنَىٰ

“Halingani sawa miongoni mwenu aliyejitolea kabla ya u shindi [wa ufunguzi wa mi wa Makkah] na akapigana, hao  watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baadae na wakapigana – na wote Allaah amewaahidi Pepo.”[2]

Wale waliojitolea na wakapambana kabla ya Ufunguzi wameahidiwa Pepo. Wale waliojitolea na wakapambana baada ya Ufunguzi wameahidiwa pia Pepo:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖتَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ ۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمْ فِي التَّوْرَاةِ ۚ وَمَثَلُهُمْ فِي الْإِنجِيلِ كَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ يُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat na mfano wao katika Injiyl kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama sawasawa juu ya shina lake liwapendezeshe wakulima ili liwaghadhibishe makafiri. Allaah amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao maghfirah na ujira mkubwa.”[3]

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na  [zikataifishwa] mali zao wanatafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake – hao ndio wakweli. Na wale waliokuwa na makazi na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohajiri kwao na wala hawapati kuhisi uzito wowote vifuani mwao kwa yale waliyopewa [Muhaajiruun] na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wako na njaa. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu. Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu vifundo vya chuki kwa wale walioamini. Ee Mola wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu.”[4]

Maadui wa Maswahabah katika Raafidhwah na Khawaarij sio ndugu wa Maswahabah. Nyoyo zao zimejaa vifundo na chuki dhidi ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Athari ya vifundo na chuki hizi walizobeba ndani ya vifua vyao zinaonekena kwenye maneno na maandishi yao. Wanawakufurisha Maswahabah, kuwalaumu na kuwatusi.

Maalik ametumia Aayah:

لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ

“… ili liwaghadhibishe makafiri.”

na:

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ

Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani.”

ili kuthibitisha ya kwamba hana haki ya kupata sehemu katika fai. Fai wanapewa wale watu tu ambao wanamuomba Allaah awawie radhi Maswahabah, anatambua nafasi yao na anawaombea:

رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ

“Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani.”

Ama kuhusu yule anayewalaani, anawatukana na kuwakufurisha hastahiki kitu katika fai. Bali mtu kama huyu anaweza hata kukufuru kwa sababu Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

لِيَغِيظَ بِهِمُ الْكُفَّارَ

“… ili liwaghadhibishe makafiri.”

Hakuna wanaowachukia isipokuwa tu makafiri.

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

“… kisha ´Umar bin al-Khattwaab halafu ´Uthmaan bin ´Affaan.”

al-Bukhaariy amepokea ya kwamba Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Tulikuwa, ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) bado yuhai,  tukizingatia ya kwamba Abu Bakr ndiye bora na halafu ´Umar, kisha ´Uthmaan. Kisha tunanyamaza.”[5]

[1] 09:100

[2] 57:10

[3] 48:29

[4] 59:08-10

[5] al-Bukhaariy (3655).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 409-411
  • Imechapishwa: 10/10/2017