Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya tisho ni maneno Yake (Ta´ala):

فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

“Basi msiwakhofu, na nikhofuni Mimi mkiwa ni waumini.” (Aal ´Imraan 03 : 175)

Tisho (Khashyah) ni khofu iliyojengwa juu ya ujuzi kutokanaa na utukufu wa yule anayemukhofu na ukamilifu wa ufalme Wake. Allaah (Ta´ala) amesema

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

“Hakika wanaomukhofu Allaah miongoni mwa waja Wake ni wanazuoni.”  (Faatwir 35 : 28)

Bi maana wanazuoni ambao wana ujuzi juu ya utukufu Wake na ukamilifu wa ufalme Wake. Tisho (Khashyah) ni aina maalum zaidi kuliko khofu (Khawf). Tofauti kati ya hayo mawili inaweza kubainika kwa mfano. Ukiwa na khofu juu ya mtu ambaye hujui aweza kukushinda au hapana, hii huhesabiwa kuwa ni khofu (Khawf). Ukiwa na khofu juu ya mtu ambaye unajua aweza kukushinda, hii inahesabiwa kuwa ni tisho (Khashyah).

Husemwa juu ya vigawanyo mbalimbali vya tisho yaleyale yanayosemwa juu ya vigawanyo vya khofu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 60
  • Imechapishwa: 25/05/2020