40. Dalili juu ya kwamba Allaah yuko juu


“Kuna mbedui alikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nafsi zinaangamia, familia zinakufa kwa njaa, wanyama wanaangamia na mali zinaharibika. Muombe Allaah atunyeshelezee. Tunakushufaia mbele ya Allaah na kwa Allaah (´Azza wa Jall) mbele yako.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ole wako! Hivi unajua unachokisema?” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kumsabihi na kumtakasa Allaah kutokamana na mapungufu mpaka hilo likatambulika nyusoni mwa Maswahabah zake. Kisha akasema: “Ole wako! Hakushufaiwi kwa Allaah mbele ya yeyote katika waja Wake. Shani ya Allaah ni kubwa kuliko hivo. Ole wako! Unamjua Allaah ni nani? ´Arshi Yake iko juu ya mbingu na ardhi Yake iko hivi” na akavifanya vidole vyake mviringo na inatoa sauti kwa sababu Yake kama mfano wa kitanda cha yule mpandaji.”[1]

Wahb akatuonyesha kwa mkono Wake.

[1] Abu Daawuud (4726) na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1547). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1017), nzuri kwa mujibu wa Ibn-ul-Qayyim katika ”Mukhtaswar-us-Sawaa´iq al-Mursalah” (3/1068).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 83-87
  • Imechapishwa: 31/03/2018