2 – Hajj ikiwa ni ya sunnah basi ni sharti kupatikane idhini ya mume wake kwa ajili ya kuhiji. Kwa sababu atapitwa na haki zake juu yake mke. Imetajwa katika “al-Mughniy”:

“Hajj ya sunnah inafaa kwa mume kumzuia. Ibn-ul-Mundhir amesema: “Wameafikiana kila yule mwanachuoni ambaye nimehifadhi kutoka kwake kwamba inafaa kwake kumzuia kwenda katika hajj iliyopendekezwa. Hayo ni kwa sababu haki ya mume ni ya lazima. Kwa hiyo mke hana haki ya kuipoteza kwa ajili ya kukiendea kitu ambacho sio cha lazima. Kama mfano wa mtumwa pamoja na bwana wake.”[1]

3 – Inasihi kwa mwanaume kumkalia niaba mwanamke katika hajj na ´umrah. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema katika “Majmuu´-ul-Fataawaa”:

“Inajuzu kwa mwanamke kumuhijia mwanamke mwingine kwa maafikiano ya wanachuoni. Ni mamoja ni msichana wake au mwengine. Kadhalika inafaa kwa mwanamke kuhijiwa na mwanaume kwa mujibu wa maimamu wanne na wanachuoni wengi. Ni kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyomwamrisha mwanamke wa Khath´amiyyah kumuhijia baba yake wakati aliposema: “Ee Mtume wa Allaah! Faradhi ya Allaah katika hajj imemkuta baba yangu akiwa ni mzee mtumzima. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha amuhijie baba yake pamoja na kuwa Ihraam ya mwanaume ni kamilifu zaidi kuliko Ihraam yake.”[2]

[1] (03/240).

[2] (26/13).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 12/11/2019