40. Aina ya kumi ya majina yaliyochukizwa


10- Kuna kundi la wanachuoni wameonelea kuchukizwa wanaume kuitwa kwa majina ya Malaika kama Jibraa-iyl, Mikaa-iyl na Israafiyl (´alayhimus-Salaam). Kuhusu wanawake kuitwa kwa majina ya Malaika, udhahiri ni kwamba ni haramu kuwapa majina ya Malaika kwa sababu ni kujifananisha na washirikina waliowafanya Malaika kuwa ni mabanati wa Allaah – Allaah ametakasika na wayasemayo! Majina yaliyo vilevile karibu na haya ni kumpa msichana jina la Malaak na Malakah.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 29
  • Imechapishwa: 18/03/2017