4. Uso ni mapambo yasiyotakikana kuonekana

Ya tatu: Allaah (Ta´ala) amekataza kabisa kuonesha mapambo isipokuwa yale yasiyoweza kufichikana kama mavazi ya nje. Ndio maana Amesema:

إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا

“… isipokuwa yale yanayodhihirika…”

Hakusema “… isipokuwa yale wanayodhihirisha…”. Kisha akakataza kuonesha mapambo kwa mara nyingine na akawachomoa wale wanaume wanaofaa kuyaona. Hili linathibitisha ya kwamba mapambo ya pili yanatofautiana na mapambo ya kwanza. Mapambo ya kwanza ni ya nje yenye kuonekana na watu wote na ambayo hakuna uwezekano wa kuyaficha. Mapambo ya pili ni yenye kufichikana ambayo anajipamba nayo. Lau mapambo haya ya pili ingelikuwa inajuzu kwa watu wote kuyaona basi kungelikuwa hakuna maana yoyote yenye kujulikana ya kufanya ujumla katika ile hali ya kwanza na umaalum katika ile hali ya pili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 8
  • Imechapishwa: 26/03/2017