4. Ukweli kuhusu al-Mu´izz al-Faatwimiy – mcheza tamthili wa al-Ikhwaan


Toleo lililotoka Rajab mlilolichapisha kwenye jarida lenu tukufu dondoo fupi kutoka kwa Ibn Kathiyr juu ya al-Mu´izz al-Faatwimiy. Hata hivyo hakukutajwa kuhusu chimbuko lake wala ´Aqiydah yake ambayo ni mchanganyiko wa ´ibaadah ya kuabudu moto, Ghanuuswiyyah na falsafa ya kiplato ya kisasa [Platonism]. Ndio maana ninataka kutimiza faida (juu ya kufichukua maadui wa Kiislamu) na kuandika kwa ufupi chimbuko hilo lililoelezwa na ´Aqiydah.

Wanahisoria waaminifu wamekubalaina juu ya kwamba chimbuko la al-Mu´izz ni la kuzushwa. Wengi wanaonelea kuwa anatokamana na Maymuun al-Qaddaah (alofariki. 261). Maymuun alikuwa ndiye kiongozi wa Qaraamitwah aliyeupiga vita Uislamu na waislamu. Dini yao ilikuwa ya kuabudu moto na huku wakidai kuwa ni waislamu. Ili kuthibitisha ukweli juu ya chimbuko lake itatosha kutaja nyaraka ya kihistoria iliotolewa na hakimu mkuu wa dola ya ´Abbaasiyyah Abu Muhammad al-Akfaaniy na ambaye alishuhudiliwa ushahidi wa kiaminifu ikiwa ni pamoja na ar-Raadhwiy ash-Shariyf, al-Murtadhwaa ash-Shariyf, Ibn-ul-Khazriy, Abu Haamid al-Asfaraayniy na Abu Ja´faar an-Nasaafiy. Kwenye nyaraka kulikuwa haya yafuatayo:

“Mashahidi wameshuhudia kwamba Ma´d ni mwana wa Ismaa´iyl mwana wa ´Abdir-Rahmaan anayejinasibisha na Dayswaan ambaye ni mwana wa Sa´iyd ambaye Dayswaaniyyah wanajinasibisha naye na kwamba ukoo huu Misri, ambaye ni Mansuur bin Nazaar, ambaye anaitwa pia al-Hakiym, ni mwana wa Ma´d ambaye ni mwana wa Ismaa´iyl ambaye ni mwana wa ´Abdir-Rahmaan na mababu walotangulia ni wachafu na manajisi – laana ya Allaah iwe juu yao na laana ya kila mwenye kulaani! Wamekuja tu na madai matupu. Hawatokamani kabisa na ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Kujinasibisha kwao kwake ni uongo na batili. Ukoo huu Misri na mababu zake ni makafiri, mazanadiki, wakanaMungu na wakanushaji. Wanakanusha Uislamu na wanahalalisha uzinzi na pombe. Wanawatukana Mitume na wanasema kuwa wana sifa za kiungu. Haya yameandikwa tarehe 01 Rabiy´ al-Awwaal 402.”

al-Mu´izz alikuwa ni kiongozi mjanja na wa khatari sana kutoka katika Ismaa´iyliyyah. Ismaa´iyliyyah ni pote lenye kuharibu ´Aqiydah ya Kiislamu. Baadhi ya sifa zao ni hizi:

1- Wanaamini kuwa baadhi ya watu wana sifa za kiungu.

2- Wanaamini kuwa baadhi ya maimamu wao wana ujumbe mkubwa kuliko ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

3- Hawafanyi makalifisho yoyote ya Kiislamu kwa vile viongozi wa kundi wanaamini kuwa Qur-aan ina maana ya uinje na maana iliyojificha. Wakimaanisha ya kwamba ile maana ya uinje ni ya jumla kwa wajinga wa waislamu na ile maana iliyojificha ni ya wasomi ambao ´ibaadah haiwawajibikii.

Waandishi: Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Wakiyl
Marejeo: Gazeti al-Hadiy an-Nabawiy (1365/7)
Mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy
Chanzo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 14-16