4- Shaykh na ´Allaamah Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)


Muheshimiwa aliulizwa swali kuhusu Shaykh Rabiy´ ambapo akasema:

“Ama kuhusu Shaykh Rabiy´, sijui juu yake isipokuwa kheri tu. Mtu huyu anafuata Sunnah na Hadiyth.”[1]

Kadhalika amesema (Rahimahu Allaah) baada ya muhadhara wa Shaykh Rabiy´ kwa jina “al-I´tiswaam bil-Kitaab was-Sunnah” aliutoa ´Unayzah, muhadhara ambao mimi mwenyewe nilifuatana na Shaykh na nikahudhuria mkutano huo:

“Kwa hakika tunamhimidi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kumrahisishia ndugu yetu Dr. Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy kutembelea mkoa huu, mpaka yule ambaye alikuwa hajui baadhi ya mambo ajue ya kwamba ndugu yetu yuko katika Salafiyyah na njia ya Salaf. Kwa kusema Salafiyyah simaanishi kipote kinachopingana na Waislamu wengine. Ninachomaanisha ni kwamba yuko katika njia ya Salaf katika mfumo wake, na khaswa inapohusiana na kuihakikisha Tawhiyd na kuilinda na yanayokwenda kinyume nayo. Sote tunajua kuwa Tawhiyd ndio asli ya wito wa Mtume ambao Allaah Amewatuma Mitume Wake (´alayhimus-Swalaat was-Salaam) nao… Bila ya shaka matembezi ya ndugu yetu Shaykh Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy katika mkoa wetu, na khaswa katika mji wetu wa ´Unayzah, yataacha athari baada yake. Kadhalika mambo mengi ambayo yalikuwa yakifichikana kwa watu wengi kupitia utahadharisho, propaganda na matamanio, yatabainika. Watu wengi wamejuta kutokamana na kuwasema vibaya wanachuoni baada ya kuona kuwa wao ndio wako katika usawa.”

Kisha msikilizaji mmoja akasema:

“Hapa kuna swali juu ya vitabu vya Shaykh Rabiy´.”

Akajibu (Rahimahu Allaah) kwa kusema:

“Dhahiri ni kwamba hakuna haja ya swali kama hili, ni kama jinsi Imaam Ahmad alivyosema wakati alipoulizwa kuhusu Ishaaq bin Raahawayh: “Mtu mfano kama mimi naulizwa kuhusu Ishaaq? Badala yake Ishaaq ndio anatakiwa kuulizwa kuhusu mimi.” Nimeshasema ninayoyajua kuhusu Shaykh Rabiy´ (Waffaqahu Allaah) na bado ninaonelea na kufikiria hali kadhalika mpaka sasa. Ujio wake kuja hapa na maneno yake yaliyonifikia hapana shaka kwamba ni miongoni mwa mambo yanayomzidishia mtu kumpenda na kumuombea du´aa.”

Vilevile aliulizwa swali lifuatalo:

“Tunajua mengi kuhusu upetukaji mpaka wa Sayyid Qutwub. Lakini kuna kitu kimoja ambacho sikukisikia kutoka kwake, bali nilisikia kutoka kwa mwanafunzi mmoja na sijakinaika nacho. Nacho inahusiana na kwamba Sayyid Qutwub ni mmoja katika wale wanaokubaliana na kauli ya Wahdat-ul-Wujuud. Hii ni kufuru. Je, Sayyid Qutwub ni katika wale wanaoamini Wahdat-ul-Wujuud? Natarajia jawabu, Allaah Akujaza kheri.

Akajibu (Rahimahu Allaah):

“Nilisoma kidogo vitabu vya Sayyid Qutwub. Sijui hali yake. Lakini hata hivyo, kuna wanachuoni ambao wameandika kuhusu kitabu chake “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan”. Wameandika makosa mengi kutoka kwenye Tafsiyr yake. Kwa mfano Shaykh ´Abdullaah ad-Duwaysh (Rahimahu Allaah) na ndugu yetu Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy ameandika makosa ya Sayyid Qutwub katika Tafsiyr yake na vitabu vingine. Kwa ajili hiyo yule anayetaka, anaweza kuvirudilia.”[2]

Aliulizwa kwenye simu kutoka Uholanzi:

“Ni ipi nasaha yako kwa anayekataza kanda za Shaykh Rabiy´ bin Haadiy kwa madai ya kwamba zinawasha fitina na kwamba zina kuwasifu watawala wa Saudi Arabia na kwamba sifa zake, yaani Shaykh Rabiy´, juu ya watawala ni unafiki?”

Jibu:

“Tunaonelea kuwa hili ni kosa kubwa. Shaykh Rabiy´ ni katika wanachuoni wa Sunnah. Ni katika watu bora. ´Aqiydah yake ni salama na mfumo wake umenyooka. Lakini, wakati alipoanza kuzungumza dhidi ya baadhi ya watu waliokuja nyuma ambao baadhi ya watu wanawachukulia kama kiigizo, wakamchafua kwa mapungufu haya.”[3]

Kadhalika aliulizwa swali lifuatalo:

“Inasemekana kwamba mfumo wa Shaykh Rabiy´ unaenda kinyume na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?”

Akajibu:

“Sijui kuwa anaenda kinyume nao. Wanachuoni wa leo wamemsifu Shaykh Rabiy´. Mimi sijui kwake isipokuwa kheri tu.”[4]

[1] Kanda ”al-As-ilah as-Swiydiyyah”.

[2] Kanda ”Liqaa´ as-Shaykh Rabiy´ m´a ash-Shaykh Ibn ´Uthaymiyn hawl al-Manhaj”

[3] Kanda ”Kashf-ul-Lithaam ´an Mukhaalafaat Ahmad Sallaam”.

[4] Kanda ”Thanaa´ A-immat-id-Da´wah ´alaa ash-Shaykh Rabiy´”

  • Mhusika: Shaykh Khaalid bin Dhwahwiy adh-Dhwafayriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.rabee.net/ar/sharticles.php?cat=12&id=57
  • Imechapishwa: 02/12/2019