4. Mtoto apewe jina la Kiislamu na kiarabu

Basi kutokana na haya ninatoa kurasa hizi nzuri kwa kila muislamu ambaye amepata mtoto wa Kiislamu ili niweze kumwelekeza katika njia inayoenda sambamba na uongofu na nuru ya Mtume na lugha ya kiarabu katika kumpa mtoto jina. Kwa hilo ana kupata ujira wa mapema kwa sababu ya kuchagua jina lililo zuri na kushikamana na Uislamu na Sunnah. Hilo linapelekea kubarikiwa yeye mwenyewe, mtoto wake na jamii yake. Kadhalika analipwa kwa kujitakasa na ujidhalilishaji wenye mabadilisho na fedheha inayopekea katika kujifananisha na majina mabaya. Pengine yakaonekana ni mazuri, lakini uhakika wa mambo yakawa na maana yenye kudharauliwa. Anajitakasa na maadili mabaya yanayoupiga vita dini yake, tabia na lugha yake na kumjaza kila aina ya mabalaa ili aache kujifakhirisha na Uislamu wake na aweze kushiriki bure kwenye mradi wenye kuudhoofisha na kuiudhi jamii yake na kusababisha kuchinjwa kwake.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 05
  • Imechapishwa: 18/03/2017