39. Vita vya uji


Abu Sufyaan akarudi Makkah baada ya utwevu uliotokea Badr. Abu Sufyaan akaweka nadhiri maji yake yasiguse maji kabla ya kwenda kumpiga vita Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akatoka na wapandaji 200 na akateremka Twaraf-ul-´Uraydhw. Akalala usiku mmoja kwa Sallaam bin Mishkam wa kabila la Banuu Nadhwiyr. Akampa vinywaji na kumpa khabari za watu. Asubuhi ilipofika akaamrisha miti midogo ya mitende ikatwe na auwawe mtu mmoja kutoka katika Answaar na awekwe badala yake mwingine. Halafu akarudi.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa tayari. Yeye pamoja na waumini wakatoka kumtafuta na wakafik katika Qarqarat-ul-Kudr, lakini Abu Sufyaan na washirikina wakawapotea. Wakachukua akiba ya kutosha kukiwemo uji na ndio maana ikaitwa ´vita vya uji`. Ilikuwa katika Dhul-Hijjah mwaka wa 2. Halafu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akarudi al-Madiynah. Wakati huo alikuwa amemwacha Abu Lubaabah katika mji kama khalifah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 54
  • Imechapishwa: 10/10/2018