Swali 39: Ni upi wakati wa mwisho wa ´Ishaa na ni vipi mtu ataujua?

Jibu: Mwisho wa wakati wa ´Ishaa ni nusu ya usiku. Mtu anajua hilo kwa kugawanya mara mbili kuanzia pale jua linapozama mpaka kuchomoza kwa alfajiri. Nusu ya mwanzo ndio wakati wa kumalizika kwa ´Ishaa. Nusu ya pili ya usiku iliyobaki sio wakati [wa ´Ishaa], bali ni nafasi kati ya ´Ishaa na Fajr.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 36
  • Imechapishwa: 06/08/2021