39. Mume amridhie mke wake


Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake ni yeye aridhie kutoka kwake yale awezayo kutoa kutokamana na tabia yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watendeeni wanawake wema. Hakika mwanamke ameumbwa kwa ubavu ulopinda. Kiungo kilichopinda zaidi kwenye ubavu wake ni kile cha juu. Ukienda kutaka kukinyoosha utakivunja, na ukikiacha kitabaki kimepinda. Hivyo basi, watedeeni wanawake wema.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema pia:

“Hakika mwanamke ameumbwa kwa ubavu ulopinda na katu hatokuwa sawa sawa vile unavotaka. Ikiwa utastarehe naye basi starehe naye ilihali huku amepinda, na ukienda kutaka kumnyoosha utamvunja; kumvunja kwake ni kule kumtaliki.”[2]

Makusudio ya haya ni mwanaume aweze kujua ni yepi maumbile ya mwanamke na aridhie kwa yale anayoyaona kutokamana na maumbile yake. Asimlazimu zaidi ya yale anayoyaweza. Awe ni mvumilivu kwa hatua yake ilopinda, kwani hakika ameumbwa kwa ubavu ulopinda.

[1] al-Bukhaariy (3331) na Muslim (1468) na muundo ni wa Muslim.

[2] al-Bukhaariy (3331) na Muslim (1468).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 56
  • Imechapishwa: 24/03/2017