Kutokana na maandiko yote na fadhila nyingi zinazoshaji´isha juu ya kuwapenda (Radhiya Allaahu ´anhum) na ukhaliyfah ulivojengeka walikuwa wakionelea kuwa Abu Bakr ndiye wa kwanza, ´Umar ndiye wa pili, ´Uthmaan ndiye wa tatu na ´Aliy ndiye wa nne. Hapo kabla Ahl-us-Sunnah walikuwa wakitofautiana ni nani bora kati ya ´Aliy na ´Uthmaan. Muda ulivyokuwa unaenda tofauti hii ikaisha na mwishowe Ahl-us-Sunnah wakaafikiana juu ya mpangilio ufuatao: Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy. Halafu wanaofuatia ni wale kumi walioahidiwa Pepo: az-Zubayr bin ´Awwaam, Twalhah bin ´Ubaydillaah, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, Sa´d bin Abiy Waqqaas, Sa´iyd bin Zayd bin ´Amr bin Nufayl na Abu ´Ubaydah ´Aamir bin Jarraah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewashuhudia Pepo na ndio maana na sisi tunashuhudia ya kwamba wataingia Peponi na tunatambua fadhila zao.

Halafu tunatambua fadhila za Maswahabah wengine waliobaki na kuthibitisha kuwa Allaah amewaahidi wote Pepo. Maswahabah wote – Allaah akitaka – wataingia Peponi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu wale walioshiriki vita vya Badr:

“Allaah amewatazama watu wa Badr na kusema: “Fanye mtakavyo. Hakika nimekusameheni”[1]

Ina maana kwamba hawatoingia Motoni kwa sababu ya msamaha huu. Kadhalika hakuna yeyote aliyekula kiapo chini ya mti ambaye ataingia Motoni:

“Hakuna yeyote atakayeingia Motoni katika wale waliokula kiapo chini ya mti.”[2]

Bi maana wale waliokuwa Hudaybiyah.

Tunawaganya Maswahabah katika mpangilio ufuatao:

1- Wale wane.

2- Wale kumi waliobaki.

3- Wale waliokula kiapo ´Aqabah.

4- Wale waliopigana vita vya Badr.

5- Wale waliokula kiapo chini ya mti.

6- Maswahabah wengine waliobaki – Allaah awawie radhi wote.

Fadhila zao zinatofautiana, kama atavyosema Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah).

[1] al-Bukhaariy (3983) na Muslim (2494).

[2] Muslim (2496) na at-Tirmidhiy (3860).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 411-412
  • Imechapishwa: 01/10/2017