Ndugu wapendwa! Tumetangulia kuzungumza kuhusu mafungu saba ya watu katika kufunga. Haya yafuatayo ni mafungu mengine yaliyobaki:

8- Mwenye hedhi. Ni haramu kwake kufunga na wala haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu wanawake:

“Sijaona walio na akili punguani na dini pungufu wanaomghalibu mwanaume mwenye busara kama nyinyi [wanawake].” Tukasema: “Ni upi upungufu wa akili na dini yetu, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Je, ushahidi wa mwanamke mmoja si ni sawa na nusu ya ushahidi mwanamme mmoja?” Tukajibu: “Ndio.” Akasema: “Huyo ndio upungufu wa akili zao.” Akasema tena: “Si wanapokuwa na hedhi si haswali na wala hafungi?”Tukajibu: “Ndio.” Akasema: “Hayo ni katika upungufu wa dini yake.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 56
  • Imechapishwa: 07/05/2020