164- ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitufunza kuanza mambo muhimu kwa:

الْحمد للهِ نَحْمَدُهُ وَنَسْتَعِينُهُ ونَسْتَغْفِره وَنَعوذُ باللهِ من شُرُور أَنْفُسِنَا وَمِنْ سَيِّئاتِ أَعْمَالِنَا مَنْ يَهْدِهِ اللهُ فَلاَ مُضِلَّ لَهُ وَمَنْ يُضْلِلْ فَلا هَادِيَ لَهُ وأَشْهَدُ أَن لا إِله إِلاَّ الله وحده لا شريك له وأَشْهَدُ أَنَّ محمداً عَبْدُهُ وَرَسُوله

“Himdi zote ni Zake Allaah. Tunamhimidi na tunamuomba msaada na msamaha. Tunaomba kinga kwa Allaah kutokana na shari ya nafsi zetu na matendo yetu maovu. Yule Aliyeongozwa na Allaah, hakuna awezae kumpoteza, na yule aliyepotezwa na Allaah, hakuna awezae kumwongoza. Nashuhudia kwamba hakuna mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, Mmoja asiyekuwa na mshirika. Nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake.”

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالًا كَثِيرًا وَنِسَاءً ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحَامَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا

“Enyi watu! Mcheni Mola wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume wengi na wanawake. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana na jamaa. Hakika Allaah Amekuwa juu yenu Raqiybaa(Mwenye kuchunga).” (an-Nisaa 04 : 01)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ

“Enyi mlioamini! Mcheni Allaah kama apasavyo kuogopwa na wala msife isipokuwa na nyinyi ni Waislamu.” (Aal ´Imraan 03 : 102)

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

“Enyi mlaomini! Mcheni Allaah na semeni kauli ya kweli (ya sawasawa). Atakutengenezeeni ‘amali zenu, na Atakusameheni madhambi yenu; na anayemtii Allaah na Mtume wake, basi kwa hakika amefanikiwa mafaniko adhimu.” (al-Ahzaab 33 : 70-71)

165- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimpongeza na kumuombea aliyeoa:

بَارَكَ الله لكَ وَبَارَكَ عَلَيْكَ وَجَمَعَ بَيْنَكُمَا فِي خَيْر

“Allaah Akubariki, Abariki juu yako na Awajumuishe katika kheri.”

166- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu akioa mwanamke au akinunua mjakazi aseme:

اللهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَهَا وَخَيْر ما جَبلتَها عَلَيْهِ وأَعُوذُ بكَ مِنْ شَرِّهَا وَشَرِّ ما جَبَلْتَها عَلَيْهِ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kheri ya huyu na kheri ya maumbile uliyomuumba nayo. Najikinga Kwako na shari yake na shari ya maumbile uliyomuumba nayo.”

Mtu akinunua ngamia basi aweke mkono wake juu ya nundu yake na kusema hali kadhalika.”

1678- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa allam) amesema:

“Pindi mmoja wenu anapotaka kumwingilia mke wake na akasema:

بسم الله اللهم جَنِّبْنَا الشَّيْطَانَ وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا

“Kwa jina la Allaah! Ee Allaah Tuepushe na Shaytwaan na muepushe Shaytwaan na ulichoturuzuku.”

Ikiwa imeshapangwa kwamba watapata mtoto basi Shaytwaan kamwe hatomdhuru.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 104-106
  • Imechapishwa: 21/03/2017