39. Dalili ya thelathini na saba kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

37- Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy ametukhabarisha: Ahmad bin al-Hasan ametuhadithia: al-Hasan bin Ahmad ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin ´Abdillaah ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad bin ´Iysaa ametuhadithia: al-Qa´nabiy ametuhadithia: Maalik ametuhadithia, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa al-A´raaj, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Salla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wanapishana kwenu Malaika wa usiku na Malaika wa mchana. Wanakusanyika katika swalah ya Fajr na swalah ya ´Aswr. Halafu hupanda wale waliolala kwenu ambapo Mola wenu Anawauliza – ilihali ni mjuzi zaidi kuliko wao: “Mmewaachaje waja Wangu?” Wanasema: “Tumewaacha na huku wanaswali na tumewaendea na huku wanaswali.”[1]

[1] al-Bukhaariy (7429) na Muslim (632).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 132
  • Imechapishwa: 18/06/2018