39. Allaah hushuka mbingu ya chini ya dunia kila usiku

Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

إلى طبقِ الدنيا يمُنُّ بفضلهِ

12 – Anashuka kuja kwenye mbingu ya dunia ili atunuku fadhilah Zake

فتفرجُ أبواب السماءِ وتُفتحُ

     milango ya mbingu hufunguliwa

يقولُ أَلا مُستغفرٌ يَلقَ غافراً

13 – Husema “Tanabahini! Kuna mwombaji msamaha akutane na mwenye kusamehe?

ومُستمنحٌ خيراً ورِزْقاً فُيمنحُ

     Je, kuna mwenye kuomba kheri na riziki ili apewe?”

MAELEZO

Anashuka kuja kwenye mbingu ya dunia. Kwa sababu mbingu ina tabaka saba. Amesema (Ta´ala):

أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا

“Je, hamuoni jinsi Allaah alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?” (71:15)

Baadhi ya tabaka ziko juu ya zingine. Hushuka (Jalla wa ´Alaa) namna anavyotaka katika mbingu ya chini inayofuatiwa na ardhi.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“… ili atunuku fadhilah Zake.”

Husema (Subhaanah):

“Je, kuna anayeniomba Nimpe?”

Hizi ni fadhilah kutoka kwa Allaah. Husema:

“Je, kuna anayeomba msamaha Nimsamehe? Je, kuna mwenye kutubia Nimkubalie tawbah yake?”

Yote haya ni  kutokana na fadhilah Zake (Subhaanahu wa Ta´ala). Anaowanyesha waja Wake ukarimu Wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Mandhuumat-ul-Haaiyyah fiy ´Aqiydati Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 101
  • Imechapishwa: 10/01/2024