39. Allaah hushuka mbingu ya chini ya dunia kila usiku


Imaam Ibn Abiy Daawuud (Rahimahu Allaah) amesema:

12- Hutunuku fadhila Zake katika tabaka ya dunia

     milango ya mbingu hufunguliwa

13- Husema “Tanabahini! Kuna mwombaji msamaha amuombae mghufiriaji

     na mwenye kuomba kheri na riziki apewe”

MAELEZO

katika tabaka ya dunia – Hushuka katika tabaka ya chini kabisa ya dunia. Kwa sababu mbingu ina tabaka saba. Amesema (Ta´ala):

أَلَمْ تَرَوْا كَيْفَ خَلَقَ اللَّـهُ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا

“Je, hamuoni jinsi Allaah alivyoziumba mbingu saba kwa matabaka?” (71:15)

Baadhi ya tabaka ziko juu ya zingine. Hushuka (Jalla wa ´Alaa) namna anavyotaka katika mbingu ya dunia inayofuatiwa na ardhi.

Hutunuku fadhila Zake… – Husema (Subhaanah):

“Kuna anayeniomba nimpe?”

Hizi ni fadhila kutoka kwa Allaah. Husema:

“Kuna anayeomba msamaha nimsamehe? Kuna mwenye kutubia nimsamehe?”

Yote haya ni  kutokana na fadhila Zake (Subhaanahu wa Ta´ala). Anawatunuku waja Wake ukarimu Wake.