al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akifasiri Aayah:

كَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah wa kati na kati.” (02:143)

“Bi maana maimamu wa kati na kati ambao ni waadilifu na wako kati na kati baina ya Mtume na watu. Dalili ya kwamba Aayah hii inawazungumzisha maimamu ni Kauli Yake katika Suurat-ul-Hajj:

لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ

“Ili Mtume awe shahidi juu yenu na [nyinyi] muwe mashahidi juu ya watu.” (22:78)

Bi maana maimamu na watakuwa mashahidi juu ya watu. Hakika iliteremshwa namna hii:

وَسَطًا أئمة جَعَلْنَاكُمْ وَكَذَلِكَ

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni maimamu wa kati na kati.””[1]

al-Qummiy amesema vilevile wakati alipokuwa akifasiri Suurat-ul-Hajj:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ ۚ فَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ وَاعْتَصِمُوا بِاللَّـهِ هُوَ مَوْلَاكُمْ ۖ فَنِعْمَ الْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ النَّصِيرُ وَجَاهِدُوا فِي اللَّـهِ حَقَّ جِهَادِهِ ۚ هُوَ اجْتَبَاكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ ۚ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَاهِيمَ ۚ هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِي هَـٰذَا

“Enyi mloamini! Rukuuni, na sujuduni na mwabuduni Mola wenu, na fanyeni [ya] kheri – huenda mkafaulu! Na pambaneni katika njia ya Allaah kama inavyostahiki kujitolea Kwake. Yeye Ndiye Amekuteueni na Hakukufanyieni ugumu wowote [ule] katika dini, dini [yenye asli] ya baba yenu Ibraahiym. Yeye Ndiye hapo kabla na katika hii [Qur-aan] Alikuiteni “Waislamu”.” (22:77-78)

“Hili linahusu tu watu wa familia ya Muhammad (´alayhis-Salaam). Kauli

لِيَكُونَ الرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ

“Ili Mtume awe shahidi juu yenu..”

Bi maana juu ya familia ya Muhammad, ama Kauli:

وَتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ

“… na [nyinyi] muwe mashahidi juu ya watu.”

Bi maana watu wa familia ya Muhammad watakuwa mashahidi juu ya watu baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Iysaa bin Maryam amesema:

وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ

“Na nilikuwa juu yao shahidi nilipokuwa nao. Uliponichukua Ulikuwa Wewe ndiye Mwenye kuchunga juu yao; na Wewe juu ya kila kitu ni Mwenye kushuhudia.” (05:117)

Vivyo hivyo Allaah Amefanya katika Ummah huu kuwepo kwa shahidi kutoka katika familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kufa kwake maadamu kuna mwenye kuishi katika dunia. Wakitoweka walimwengu wanaangamia. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah Amezifanya nyota kuwa ni zenye kuleta usalama kwa viumbe wa mbinguni na Akafanya watu wa familia yangu kuleta usalama kwa walimwengu.””[2]

1- Kuhusiana na kauli yake “Hakika iliteremshwa namna hii:

وَسَطًا أئمة جَعَلْنَاكُمْ وَكَذَلِكَ

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni maimamu wa kati na kati.””

Aayah hii inamzungumzisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Ummah wake na khaswa Maswahabah zake watukufu. Aayah hii haiwazungumzishi kabisa maimamu kwa sababu walikuwa bado hawajapatikana.

Pili ni kumsemea uongo Allaah na kumkadhibisha ambaye Amesema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi Tumeteremsha hii Qur-aan na hakika Sisi bila shaka ndio Tutakaoihifadhi!” (15:09)

Tatu ni kuwazulia Maswahabah uongo na kuwatuhumu kuwa wameipotosha Qur-aan.

Nne ni kutukana Ummah mzima juu ya kwamba Qur-aan imehifadhiwa kuongezwa na kupunguzwa.

2- Aayah hii inathibitisha fadhila za Ummah huu na ubora wake juu ya nyumati zingine zote. Allaah (Ta´ala) Amesema:

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ

“Mmekuwa Ummah bora kabisa uliotolewa [mfano] kwa watu.” (03:110)

Ummah kuwa wa kati na kati makusudio ni kwamba ni waadilifu na Allaah Anakubali ushahidi wao juu ya wengine. Neno “wa kati na kati” kulifasiri ya kwamba ni familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wao ndio wakati na kati baina ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) watu ni upotoshaji na ni kumsemea uongo Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na njia fulani ya kuunyima Ummah hadhi yake. Hata hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifasiri neno hilo. Imaam Ahmad amepokea kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusiana na Kauli Yake (Ta´ala):

كَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah wa kati na kati.”

“Bi maana waadilifu”[3]

Imaam Ahmad amepokea kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Siku ya Qiyaamah Nuuh ataitwa na kuulizwa: “Je, ulifikisha?” Atasema: “Ndio”. Hapo ndipo kutaitwa Ummah wake na kuulizwa: “Je, mlifikishiwa?” Watasema: “Hatukujiwa na mwonyaji yeyote. Hakuna aliyetujia.” Halafu Nuuh ataambiwa: “Ni nani atayekutolea ushahidi?” Atasema: “Muhammad na Ummah wake.” Hiyo ndio maana ya Kauli Yake (Jalla Dhikruh):

كَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah wa kati na kati.” (02:143)

Wa kati na kati maana yake ni waadilifu. Mtaitwa mtoe ili mtoe ushahidi wa ufikishaji wake. Kisha mimi nitatoa ushahidi juu yenu.”[4]

Aayah katika Suurat-ul-Hajj inazidi kutilia nguvu yaliyothibitishwa kwenye Kauli ya Allaah (Ta´ala):

كَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah wa kati na kati.”

Hadiyth aliyoitaja ni batili kwa sababu inaenda kinyume na maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya fadhila na hadhi ya Maswahabah pale aliposema:

“Nyota ni usalama wa mbingu. Nyota zikipotea mbingu inafikwa na kile ilichoahidiwa. Mimi ni usalama wa Maswahabah zangu. Nikipotea Maswahabah zangu watafikwa na kile walichoahidiwa. Na Maswahabah zangu ni usalama wa Ummah wangu. Pindi Maswahabah zangu watapopotea Ummah wangu utafikwa na kile walichoahidiwa.”[5]

Ni wingi wa fadhila zilizoje walonazo Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo ziko juu na imara kuliko minyororo ya mlima! Uongo wa Raafidhwah na wafuasi wao hawatoiondosha.

[1] Tafsiyr al-Qummiy (1/63).

[2] Tafsiyr al-Qummiy (2/88).

[3] Ahmad (3/9).

[4] Ahmad (3/32), al-Bukhaariy (4487), at-Tirmidhiy (2921), an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.

[5] Muslim (2531) na Ahmad (4/399).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 71-73
  • Imechapishwa: 19/03/2017