39. Aina ya tisa ya majina yaliyochukizwa

9- Aina ya tisa ya majina yaliyochukizwa ni yale majina yaliyo pamoja kama Muhammad Ahmad na Muhammad Sa´iyd. Katika hali hii Ahma ndio jina ilihali Muhammad liko kwa dhumuni la kutabaruki. Majina kama haya yanasababisha utatizi na ndio maana hayakuwa yakitambulika wakati wa Salaf. Yamejitokeza katika karne zilizokuja nyuma.

Vivyo hivyo inahusiana pia na majina yaliyo na jina “Allaah” kama Hasbullaah, Rahmatullaah na Jabrullaah. Katika hayo kunavuliwa “´Abdullaah” kwani ndio jina linalopendwa zaidi na Allaah.

Hali kadhalika inahusiana na majina yaliyo na Mtume kama Hasb-ur-Rasuul na Ghulaam-ur-Rasuul.

  • Mhusika: ´Allaamah Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasmiyat-ul-Mawluwd, uk. 28
  • Imechapishwa: 18/03/2017