38. Mume apuuzie mapungufu ya mke na mazuri yake ayafanye makubwa

Miongoni mwa haki za mke juu ya mume wake ni asimchukize. Asiangalie mapungufu yake. Anachotakiwa ni kuangalia mazuri yake, ayafanye kuwa ni makubwa na mapungufu yake ayachukulie wepesi. Afanye kila aliwezalo asione jengine kutoka kwake isipokuwa tu yale ambayo ni mazuri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini mwanaume asimchukie muumini mwanamke. Akichukia moja katika tabia yake, basi atapenda [tabia yake] nyingine.”[1]

[1] Muslim (1469).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 55-56
  • Imechapishwa: 24/03/2017