38. Makatazo ya kuzama sana ndani kwenye sifa za Allaah

38- Imaam ´Umar bin Ibraahiym ametuhadithia: Bishr ametuhadithia, kutoka kwa Ahmad: al-Haytham bin Khalaf ametuhadithia: Bishr bin al-Waliyd ametuhadithia… ح Muhammad bin Muhammad bin ´Abdillaah bin Mahmuud ametuhadithia: Muhammad bin al-´Abbaas al-´Ismiy ametuhadithia: Muhammad bin Mu´aadh ametuhadithia ya kwamba al-Firyaabiy amemuhadithia… ح ´Umar bin Ibraahiym ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Umar al-Juwaybiriy ametuhadithia: Ahmad bin Muhammad al-Kushmayhiniy ametuhadithia: al-Firyaabiy ametuhadithia: ´Aliy bin Thaabit ametuhadithia: al-Wazzaa´ bin Naafiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Saalim bin ´Abdillaah, kutoka kwa baba yake (Radhiya Allaahu ´anh) aliyeeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fikirieni alama za Allaah (´Azza wa Jall) na wala msimfikirie Allaah (´Azza wa Jall).”[1]

[1] Ibn ´Adiy (3/2/138), at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Awsatw” (6315), Abuush-Shaykh katika ”al-´Adhwamah” (1/2 – nuskha asili ya mwandishi), al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan” (1/1/35), al-Aswbahaaniy katika ”at-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2/174 – nuskha asili ya mwandishi) na ad-Daylamiy (108 – nuskha asili ya mwandishi). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3/49). as-Sakhaawiy amesema:

”Mlolongo wa wapokezi wake ni dhaifu, lakini pindi zinapokusanywa zote zinakuwa na nguvu. Lakini hata hivyo maana yake ni sahihi.” (al-Maqaaswid al-Hasanah, uk. 159)

  • Mhusika: Imaam Abu Ismaa´iyl ´Abdullaah bin Muhammad al-Answaariy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Arba´uun fiy Dalaa-il-it-Tawhiyd, uk. 77
  • Imechapishwa: 14/02/2017