38. Inajuzu kuwasengenya Ahl-ul-Bid´ah?

Swali 38: Inajuzu kuwasengenya Ahl-ul-Bid´ah? Uasi unaoendelea hii leo Algeria ina maana kila anayefanya uasi katika wao anazingatiwa kuwa ni katika Khawaarij au sivyo?

Jibu: Ni jambo lisilo na shaka kwamba kuwaongelea Ahl-ul-Bid´ah inajuzu. Kwa sharti lengo iwe ni kutahadharisha juu ya Bid´ah zao. Kama mnavyojua kusengenya kumevuliwa mambo sita:

La kwanza: Kutahadharisha.

La pili: Kunapojibiwa swali.

La tatu: Mdhulumiwa.

La nne: Anayedhihirisha maasi.

La tano: Kuarifisha.

La sita: Anayeomba usaidizi juu ya kuondosha maovu.

Ikiwa makusudio ya kuwaongelea Ahl-ul-Bid´ah ni kutaka kubainisha Bid´ah zao, kuzitahadharisha na [kumtahadharisha] yule aliyetumbukiaemo, hakuna neno. Ama endapo malengo itakuwa kutaka kukiuka heshima za watu, haijuzu.

Ama kuhusu wale walioingia Algeria hawakuwaua waislamu isipokuwa baada ya kuwakufurisha. Kuhusu yale mauaji na ukatili wa pamoja tunaosikia kwenye vyombo vya khabari na magazeti, hakika wao kwa matendo haya wameichafua sura ya Uislamu. Tunamuomba Allaah awafanye kile wanachostahiki.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017