38. Dalili ya thelathini na sita kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


36- Muhammad ametukhabarisha: Ahmad ametuhadithia: Haafidhw Abu Nu´aym ametuhadithia: Abu Bakr bin Khallaad ametuhadithia: al-Haarith bin Abiy Usaamah ametuhadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: al-A´mash ametuhadithia, kutoka kwa Ibraahiym at-Taymiy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abu Dharr (Radhiya Allâhu ´anh) ambaye amesema:

“Tulikuwa tumeketi kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) msikitini wakati jua lilipozama. Akasema: “Ee Abu Dharr! Je, unajua ni wapi jua linapozamia?”Nikajibu: “Allaah na Mtume wake ndio wajuzi zaidi.” Akasema: “Linaenda mpaka linasujudu chini ya ´Arshi kwa Mola wake na linaomba idhini. Linaomba idhini na halipewi idhini mpaka lishufai na kutaka. Baada ya muda mrefu ndio huambiwa: “Chomoza sehemu yako.” Hiyo ndio tafsiri ya maneno Yake (Ta´ala):

وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ

“Jua linatembea hadi matulio yake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu kabisa, Mjuzi wa yote.”[1][2]

[1] 36:38

[2] al-Bukhaariy (3199) na Muslim (159).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 18/06/2018