38. Dalili juu ya Kursiy ya Allaah

37- Abu Bakr al-Aadamiy Ahmad bin Muhammad bin Ismaa´iyl al-Muqri’ ametuhadithia: Ahmad bin Mansuur bin Sayyaar ametuhadithia: Yahyaa bin Bukayr ametuhadithia: Israa’iyl ametuhadithia, kutoka kwa Abu Ishaaq, kutoka kwa ´Abdullaah bin Khaliyfah, kutoka kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesema:

“Kuna mwanamke alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Niombee kwa Allaah (´Azza wa Jall) aniingize Peponi.” Akamuadhimisha Mola (´Azza wa Jall) kisha akasema: “Kursiy Yake imeenea mbinguni na ardhini. Kwa sababu ya utizo wake inatoa sauti kama kitanda kipya cha ngamia.”[1]

[1] Jaami´-ul-Bayaan (4/540) ya at-Twabariy, as-Sunnah (1/301) ya ´Abdullaah bin Ahmad, as-Sunnah (1/251) ya Ibn Abiy ´Aaswim na Naqdhu ´Uthmaan bin Sa´iyd ´alaa al-Mariysiy al-Jahmiy al-´Aniyd (1/425) ya ad-Daarimiy.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 77-79
  • Imechapishwa: 03/03/2018