38. Anayetokwa na utoko kuswali kisimamo cha usiku kwa wudhuu´ wa ´Ishaa


Swali 38: Je, inafaa kwa mwanamke huyu anayetokwa na utoko[1] kuswali kisimamo cha usiku kukipita nusu ya usiku kwa wudhuu´ wa swalah ya ´Ishaa?

Jibu: Hapana. Ukishapita nusu ya usiku basi itamlazimu kutawadha upya. Yako maoni mengine yanayosema pia kwamba si lazima kutawadha upya, nayo ndio maoni yenye nguvu.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/37-anayetokwa-na-utoko-kukaa-na-wudhuu-muda-mrefu/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 02/08/2021