Swali 38: Nisiposwali swalah ya ijumaa pamoja na wengine msikitini niiswali Rak´ah mbili nyumbani kwa nia ya ijumaa au niiswali Rak´ah nne kwa nia ya Dhuhr[1]?

Jibu: Ambaye hakuhudhuria swalah ya ijumaa pamoja na waislamu kutokana na udhuru unaokubalika katika Shari´ah, kama vile maradhi au sababu nyenginezo, basi ataiswali Dhuhr. Vivyo hivyo mwanamke ataswali Dhuhr. Hali kadhalika msafiri na wakazi wa jangwani wataswali Dhuhr. Hivo ndivo inavyojulisha Sunnah. Hayo ndio maoni ya wanazuoni wote na wala hakuna mazingatio kwa wale waliotofautiana nao. Kadhalika kwa yule ambaye ameiacha kwa makusudi anatakiwa kutubu kwa Allaah na aiswali Dhuhr.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/332).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 77
  • Imechapishwa: 04/12/2021