38. al-´Ayyaashiy upotoshaji wa kumi na moja wa al-Baqarah

Allaah (Ta´ala) Amesema:

صِبْغَةَ اللَّـهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ

“Dini ya Allaah na ni dini yepi amabyo ni bora zaidi kuliko dini ya Allaah? Na sisi ni wenye kumwabudu Yeye pekee.” (02:138)

al-´Ayyaashiy amesema:

“Kutoka kwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz bin Kathiyr al-Haashimiy, mtumwa wa Abu Ja´faar, ameeleza kuwa Abu ´Abdillaah amesema kuhusiana na Kauli ya Allaah:

صِبْغَةَ اللَّـهِ ۖ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ صِبْغَةً ۖ وَنَحْنُ لَهُ عَابِدُونَ

“Dini ya Allaah na ni dini yepi amabyo ni bora zaidi kuliko dini ya Allaah? Na sisi ni wenye kumwabudu Yeye pekee.”

“Dini ni kumtambua kiongozi wa waumini kwa mapenzi ya mkataba.”[1]

Utafikiri ni Raafidhwah peke yao ndio wana hadhi hii kinyume na Maswahabah watukufu na wale wenye kuwaigiza. Kwa mujibu wa uelewa huu ina maana wamekufuru kwa kutomtambua kiongozi wa waumini kwa mapenzi ya mkataba.

[1] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/62).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 71
  • Imechapishwa: 19/03/2017