37. Unasemaje juu ya Khawaarij watadumishwa Motoni milele?

Swali 37: Je, Khawaarij watadumishwa Motoni milele? Je, matendo yao ni yenye kuwatoa katika Uislamu au wataadhibiwa kwa kiwango cha matendo yao na mwisho wao itakuwa Peponi? Je, wanaingia katika mapote sabini na mbili aliyotaja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au sivyo?

Jibu: Haya yamejengwa juu ya maoni yanayoonelea kuwa ni makafiri au sio makafiri. Iwapo tutasema kuwa ni makafiri basi hiyo ina maana kuwa watadumishwa Motoni milele kama watavyodumishwa makafiri. Na endapo tutasema kuwa sio makafiri – lakini wana ukafiri mdogo – hapa tutasema kuwa hukumu yao ni kama ya wale waislamu wataoingia Motoni kwa sababu ya kufanya madhambi na halafu baada ya hapo watatolewa na kuingizwa Peponi baada ya wao kusafishwa. Hata hivyo watabaki humo kwa muda mrefu unaojua Allaah Pekee.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Jaliyyah
  • Imechapishwa: 23/07/2017