37. Tofauti kati ya Mu´awwilah na Mufawwidhwah

Wale wenye kuonelea kuwa hazitakiwi kupitishwa kama zilivyo na wakakanusha sifa za Allaah zilizothibiti au baadhi yake au wakathibitisha hali tofauti na sifa, ni makundi mawili:

1- Mu´awwilah katika Jahmiyyah na wengineo. Wameyafasiri kimakosa maandiko ya sifa kwa maana walizoziteua wao. Kwa mfano wamefasiri mkono kuwa ni neema, kulingana kwamba ni kutawala na mfano wa hayo.

2- Mufawwidhwah. Ni wale wanaosema kuwa Allaah pekee ndiye anayejua maana ya maandiko. Halafu wanasema kuwa haziwezi kuwa na maana ya kidhahiri. Huku ni kujigonga. Kudai namna hii baada ya kusema kwamba hawajui zina maana gani ni kujigonga. Katika hali kama hii hawatakiwi kuthibitisha wala kukanusha, jambo ambalo liko wazi.

Tofauti kati ya makundi haya mawili, ni kwamba hilo la kwanza wanathibitisha maana inayoenda kinyume na ile ya dhahiri, wakati hilo la pili wanaitegemeza maana kwa Allaah pasi na kuthibitisha maana yoyote. Pamoja na hivyo wanaona kwamba maandiko hayo hayamthibitishii sifa yoyote Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 87-88
  • Imechapishwa: 13/05/2020