37. Mambo ya kuzingatia wakati wa kumuosha maiti

29- Wakati wa kumuosha inatakiwa kuchunga mambo yafuatayo:

1- Kumuosha mara tatu au zaidi ya hapo kutokana na vile watavyoona wale wenye kumuosha.

2- Majosho iwe kwa witiri.

3- Baadhi ya majosho hayo yachanganywe na mkunazi na kitu kinachokaa mahala pake katika vitu vyenye kusafisha, kama mfano wa mti wa ukoka na sabuni.

4- Achanganye pamoja na josho la mwisho kitu katika mafuta mazuri ingawa kafura ndio bora zaidi.

5- Kufumua misuko na kuziosha vizuri.

6- Kuchanua nywele.

7- Kuzifanya mikia mitatu – kwa mwanamke – na kuzitupia nyuma yake.

8- Kumuanza zile pande za kuliani na vile viungo vya wudhuu´.

9- Mvulana asimamiwe kuoshwa na wanaume na msichana wanawake – isipokuwa yale yaliyobaguliwa kama ambavyo utakuja ubainifu wake.

Dalili ya mambo haya ni Hadiyth ya Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia na sisi tuko tunamuosha msichana wake [Zaynab] ambapo akasema: “Muosheni mara tatu, au mara tano [au mara saba] au zaidi ya hivo mkiona kufanya hivo kwa maji na mkunazi. [Nikasema: “Witiri?” Akajibu: “Ndio] na mjaalie mara ya mwisho kafura au kitu katika kafura. Mtapomaliza basi nijuzeni. Tulipomaliza tukamjuza ambapo akatutupia kikoi chake na akasema: “Hiki kiwe cha kwanza katika kumvisha [akimaanisha kikoi chake]. [Tukazifumua mikia mitatu]. [Katika upokezi mwingine imekuja: “Tukazichanua kisha tukaziosha]. [Tukazisuka mikia mitatu: msuko mmoja upande wa kulia, mwingine upande wa kushoto na mwingine katikati yake] na tukazitupilia kwa nyuma yake]. [Akasema: “Anzeni kwa pande zake kulia na zile sehemu zake za wudhuu´].

Ameipokea al-Bukhaariy (03/99-104), Muslim (03/47-48), Abu Daawuud (02/60-61), an-Nasaa´iy (01/266-267), at-Tirmidhiy (02/130-131), Ibn Maajah (01/445), Ibn Jaaruud (258-259), Ahmad (05/85, 4076-408). at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Hivi ndivo wanavofanya wanachuoni.”

Upokezi wa pili ni wa al-Bukhaariy na an-Nasaa´iy. Ziada ya kwanza ni ya Muslim, ziada ya pili ni yake na ya al-Bukhaariy, ya Abu Daawuud na ya an-Nasaa´iy. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea Hadiyth yenye maana yake. Ziada ya nne ni ya al-Bukhaariy na Abu Daawuud na ya tano ni yake, ya Muslim, ya an-Nasaa´iy, ya Ibn Maajah na ya Ahmad. Ziada ya sita ni ya al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad. Ziada ya saba ni ya al-Bukhaariy, ya Abu Daawuud, ya an-Nasaa´iy na ya Ahmad. Ziada ya mwisho ni ya wote hao.

10- Aoshwe kwa kutumia kitambara au kitu mfano wake chini ya kitu kinachositiri mwili wake baada ya kumvua nguo zake zote. Hivo ndivo ilivyokuwa inafanywa wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama inavyofidisha Hadiyth ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Pindi walipotaka kumuosha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walisema: “Tunaapa kwa Allaah kwamba hatujui kama tumvue nguo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama tunavyowavua nguo maiti wetu au tumuoshe akiwa na nguo zake? Wakati walipotofautiana Allaah aliwatupia usingizi kiasi cha kwamba hapakuweko yeyote isipokuwa kidevu chake kilikuwa kifuani mwake. Kisha wakazungumzishwa na mzungumzaji kutoka katika umoja wa upande wa nyumba – na hawajui ni nani: “Muosheni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa na nguo zake.  Wakasimama kumwelekea Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakamuosha akiwa na kanzu yake ambapo wanamwaga maji juu ya ile kanzu na wakimsugua kwa ile kanzu pasi na mikono yao (kugusa mwili wake). ´Aaishah alikuwa akisema: “Lau ningeliamua kuliendea jambo langu basi nisingelirudi nyuma; asingelioshwa isipokuwa na wake zake.”

Ameipokea Abu Daawuud (02/60), Ibn Jaaruud  katika “al-Muntaqaa” (257), al-Haakim (03/59-60) na ameisahihisha juu ya sharti za Muslim. Vilevile ameipokea al-Bayhaqiy (03/387), at-Twayaalisiy (nambari. 1530), Ahmad (06/267) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Ameipokea pia Ibn Maajah (01/446) kwake ndiko kumetoka maneno ya ´Aaishah mwishoni mwake:

“Lau ningeliamua kuliendea… “

Vilevile ameipokea Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (01/446).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 17/02/2020