225- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuweni na haya kwa Allaah ukweli wa kuwa na haki.” Tukasema: “Ee Mtume wa Allaah! Hakika sisi tunamstahiki Allaah na himdi zote ni Zake.” Akasema: “Simaanshi hivo. Kuwa na haya kwa Allaah ukweli wa kuwa na haya namaanisha kukihifadhi kichwa chako na vyote inavyofanya na tumbo na vyote inavyofanya na uyakumbuke mauti na mitihani. Anayeitaka Aakhirah basi atayaacha mazuri ya dunia hii. Mwenye kufanya hivo ndiye ambaye yuko na haya kwa Allaah ukweli wa kuwa na haya.”[1]

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَّهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا

“Hakika Sisi tumefanya vilioko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili Tuwajaribu ni nani miongoni mwao mwenye ‘amali nzuri kabisa.” (18:07)

الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا

“Mali na watoto ni pambo la uhai wa dunia. ‘Amali njema zibakiazo ni bora mbele ya Mola wako kwa thawabu na matumaini.” (18:46)

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ

“Watu wamepambiwa kupenda matamanio miongoni mwa wanawake, na watoto na mirundi ya mali iliyorundikwa ya dhahabu na fedha na farasi wenye chapa na wanyama wa mifugo na mashamba – hayo ni starehe za uhai wa dunia na Allaah Kwake kuna marejeo mazuri.” (03:14)

226- Tuyaangalie haya kwa mtazamo wa Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mali hii ni kijani kibichi. Allaah amewapeni nayo urathi ili aangalie namna gani mtatenda.”[2]

227- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kikubwa kinachokukhofieni kwenu ni vile vizuri vya dunia ambavyo Allaah atakutoleeni.” Kukasemwa: “Ni vyepi hivyo vizuri vya dunia?” Akasema: “Baraka za ardhi.”[3]

Hii ina maana ya kwamba dunia hii ni tamu na inaonekana vizuri. Ni kama tende tamu na ilio nzuri. Allaah anawapa waja Wake majaribio kwayo ili atazame ni nani katika wao atayetenda vyema zaidi na ambaye ni mwenye kuipa nyongo zaidi.

[1] at-Tirmidhiy (2458), Ahmad (1/387) na al-Haakim (4/323) ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

[2] Muslim (2742).

[3] al-Bukhaariy (4/69) na Muslim (1052).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Ahmad al-Qurtwubiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Hirsw biz-Zuhd wal-Qanaa´ah, uk. 132-134
  • Imechapishwa: 18/03/2017