37. Kuwaombea wanandoa watoto wengi wa kiume ni mambo ya Jaahiliyyah

35- Kuwaombea wanandoa watoto wengi wa kiume na msemo wakati wa kipindi cha kikafiri

Haitakiwi kusema “Ujaaliwe watoto wengi wa kiume”, kama wanavofanya wale wasiojua. Kwani hayo ni katika matendo ya kipindi cha kikafiri, na ni jambo limekatazwa katika Hadiyth nyingi ikiwa ni pamoja na:

al-Hasan (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba ´Uqayl bin Abiy Twaalib mwanamke kutoka katika kabila la Jashm. Watu wakaja nyumbani kwake na kusema: “Ujaaliwe watoto wengi wa kiume.” ´Uqayl akasema: “Usiseme hivo, kwani Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo.” Wakasema: “Tuseme nini, ee Abu Zayd?” Akasema: “

بارك الله لكم وبارك عليكم

“Allaah akubariki na abariki juu yenu.”

hivyo nivyo tulivyokuwa tukiamrishwa[1].

[1] Ameipokea Ibn Abiy Shaybah (02/52/07), ´Abdur-Razzaaq katika “al-Muswannaf” yake (06/189/10457), an-Nasaa´iy (02/91), Ibn Maajah (01/589), ad-Daarimiy (01/134), Ibn Abiy ´Aaswim katika “Aahaad” (02/37) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aadaab-uz-Zafaaf, uk. 175-176
  • Imechapishwa: 27/03/2018