7- Mgonjwa ambaye kuna matarajio ya kupona maradhi yake. Mgonjwa kama huyu anazo hali tatu:

1- Swawm si nzito kwake na wala haimdhuru. Huyu ni lazima kwake kufunga kwa sababu hana udhuru wowote unaomhalalishia kula.

2- Swawm ni nzito kwake lakini haimdhuru. Huyu atakula. Amesema (Ta´ala):

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.”[1]

Imechukizwa kwake kufunga ikiwa anahisi uzito. Kwa sababu ni kutoka nje ya ruhusa ya Allaah (Ta´ala) na ni kuiadhibu nafsi yake. Imepokelewa katika Hadiyth:

“Allaah anapenda zitendewe kazi ruhusa Zake kama anavochukia kutendewa kazi maasi Yake.”

Ameipokea Ahmad, Ibn Hibbaan na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh zao wawili hao”[2].

3- Swawm ikamdhuru. Ni lazima kwake kula na wala haijuzu kwake kufunga. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا

“Wala msiziue nafsi zenu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwahurumia.”[3]

وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ

“Wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo.”[4]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika nafsi yako ina haki juu yako.”

Ameipokea al-Bukhaariy.

Miongoni mwa haki zake ni wewe usiidhuru kunapokuwa kuna ruhusa ya Allaah (Subhaanah). Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna madhara wala kudhuriana.”

Ameipokea Ibn Maajah na al-Haakim. an-Nawawiy amesema:

“Inazo njia zinazopeana nguvu.”

[1] 02:185

[2] Lakini cheni ya wapokezi wake kuna kitu katika mgongano. Lakini ina shawahidi kutoka katika Hadiyth na misingi ya Kishari´ah.

[3][3] 04:29

[4] 02:195

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 53
  • Imechapishwa: 05/05/2020