Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

35- Wote wanaendeshwa na matakwa ya Allaah, baina ya fadhilah Zake na uadilifu Wake.

MAELEZO

Hakuna mja yeyote anayetoka nje ya utashi wa Allaah. Baadhi wanapata fadhilah Zake, bi maana wale wenye kufanya mazuri na wenye kutii. Wengine wanapata uadilifu Wake, bi maana makafiri na washirikina. Haya ndio yenye kulingana na hekima na utukufu Wake (Subhaanah). Hakusanyi kati ya vinyume viwili na vyenye kutofautiana viwili. Bali anakiweka kila kimoja mahala pake stahiki. Kwa ajili hiyo miongoni mwa majina Yake ni الحكيم, Mwingi wa hekima. Hekima ni moja katika sifa Zake. Mwenye hekima ni yule mwenye kukiweka kila kitu mahala pake stahiki. Anawatukuza wema kwa fadhilah na anawaadhibu makafiri na watenda madhambi. Hii ni fadhilah na uadilifu Wake (Subhanaah).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 54
  • Imechapishwa: 26/09/2019